Wazo Bora Pitch ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya vijana wajasiriamali wenye ulemavu nchini Tanzania, likiwaangazia wafanyabiashara wabunifu ambao wako tayari kukua na kupanua biashara zao.

Muombaji/Waombaji watakaofanikiwa kufika hatua ya kuchaguliwa:

  • Utapata nafasi ya kuwasilisha mawazo ya biashara yako mbele ya jopo la wataalamu.
  • Utapata nafasi ya kujulikana
  • Mrejesho wa kitaalamu kwenye wazo lako, na
  • Msaada maalum utakaoisaidia biashara yako kukua na kuimarika.

Sifa na vigezo vya washiriki/Mshiriki

  • Vijana/Kijana mwenye ulemavu umri kati ya miaka 18 mpaka 40
  • Biashara amabzo zimekuwa endelevu kwa angalau kwa miezi sita
  • Biashara zinazo patikana au endeshwa ndani ya Dar es Salaam.

Kumbuka Majibu yako yatatusaidia kukujua wewe na biashara yako kwa undani. Tafadhali hakikisha unajaza vipengele vyote vya fomu kwa usahihi ili kurahisisha mchakato wa uchambuzi.