Maombi ya Ushiriki katika Mradi wa uwezeshaji kiuchumu_RISE/E Futuremakers Tanzania

YoWDO kwa kushirikiana na Sightsavers tunawaalika vijana wenye ulemavu wa kike na wakiume wenye miaka 18-35 wanaoishi mkoa wa Dar es Salaam kutuma maombi ya kushiriki kwenye Mradi wa Ready for Inclusive Sustainable employment and entrepreneurship (RISEE)

Sifa za lazima ili kushiriki kwenye Mradi

. Vijana wa kike na vijana wa kiume wenye ulemavu wanaoishi mkoa wa Dar es Salaam 

• Umri wa miaka 18-35 wakati wa kutuma maombi 

• Elimu: Wahitimu wa Sekondari, Vyuo vya kawaida, Vyuo Vikuu na Elimu ya Ufundi stadi

• Uelewa wa lugha ya kiingereza.

Kumbuka: Kama uliwahi kushiriki Cohort (Awamu) zilizopita huruhusiwi kuomba tena au kama uliwahi kusoma course za Accenture hutokubaliwa kushiriki.